Latest Updates

Best Nasso - Nitarudi Morogoro [Official Music Video]

Ommy Dimpoz - Wanjera (Official Video HD)

MAHAKAMA YAAMURU FAMILIA YA MARVIN GAYE KULIPWA FIDIA

Mahakama nchini Marekani imetoa uamuzi kuwa mwandishi wa wimbo wa Blurred lines, ambayo ni singo iliyouza mno, aliiba mashairi ya wimbo wa Marvin Gaye. Jopo la wazee wa mahakama Jijini Los Angeles limesema singo hiyo ya mwaka 2013 iliyoimbwa na Pharrell Williams na Robin Thicke imevunja sheria za hati miliki kwa kuiba mashairi ya wimbo Got To Give It Up wa Gaye alioutoa mwaka 1977. Kutokana na kosa hilo mahakama imeamuru familiya ya marehemu Mravin Gaye, kulipwa dola milioni 7.3 kama fidia. Hata hivyo Thicke na Williams wamekanusha kuiga traki hiyo kali na wakili wao amesema uamuzi huo wa mahakama ni wa kutisha by Zourha Malisa

MWANAMKE ALIYE NA SURA YA AINA YAKE AACHIA FILAMU YAKE

Mwanamke anayedaiwa kuwa na sura mbaya duniani na mitandao inayomuonea ametoa filamu kuhusu maisha yake. Maisha ya Lizzie Velasquez mwenye umri wa miaka 26 yalibadilika kabisa baada ya kuona kanda ya video katika mtandao wa tube iliodai kwamba yeye ndiye mwanamke mwenye sura mbaya duniani. Lizzie ambaye alikuwa na miaka 17 wakati huo alikasirishwa kuona kwamba msichana aliyekuwa katika kanda hiyo ya video alikuwa yeye. Kanda hiyo ilioonekana mara millioni 4 mtandaoni huku wengi wakiwacha ujumbe wa kuudhi kama vile ''angeuliwa alipozaliwa'',nilishangaa nilipoona ujumbe huo alisema Lizzie.
Ujumbe mwengine ulisoma ''kwa nini wazazi wake walimlea''. Mwanamke huyo alipiga moyo konde na kuanza mtandao wake wa You Tube akiwaelezea watu kuhusu mwanamke huyo anayedaiwa kuwa mwenye sura mbaya zaidi. Lizzie amesema kuwa anawasaidia wengine ambao wamekuwa wakionewa kuweza kupata msaada ama hata kupambana na maonevu hayo. Mwanamke huyo pia anafanya kazi na Tina Meir ambaye mwana wao Mega alijiuwa baada ya kuonewa katika mtandao. By Pro24

Jose Chameleone Ft:Patoranking - Only You (2015) (Official Audio)

Hii ni Good news kutoka kwa Ay, Shaa, Fid Q na Sauti Soul Mwaka 2015

Wakali kutokea Tanzania, Fareed Kubanda aka Fid Q, Shaa pamoja na A.Y wakiwa bado wapo nchini Kenya wameingia studio na kundi la Sauti sol kurekodi single mpya. Kupitia kwenye Instagram, Sauti Sol wamepost dakika chache zilizopita na kuandika; “Last night we were part of something phenomenon.It was great working with true artists lyrical geniuses. @aytanzania @shaa_tz @bienaimesol @fancy_fingers @iamchimano“– @sautisol

Taarifa iliyonifikia kuhusu MBUNGE aliyefariki leo TANZANIA

Mbunge wa Mbinga na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa CCM, Kapteni John Komba amefariki leo, taarifa iliyotolewa kwenye ukurasa wa Twitter wa Chama cha CCM, hajawamesema chanzo cha kifo chake. Katika Tweet hiyo imeandikwa kwamba Mbunge huyo amefariki akiwa hospital ya TMJ. Marehemu Kapteni Komba alikuwa kiongozi wa bendi ya TOT. Naendelea kufuatilia taarifa hii na kila kitakachonifikia nitakuwa nakufahamisha pia hapahapa. RIP Kapteni Komba.

Picha 11 za jinsi huyu anaetuhumiwa kuwa tapeli anaetumia jina la Jokate Mwegelo alivyokamatwa

Aliefanikisha huyu jamaa kukamatwa ni mrembo mmoja model Blessing ambae alishiriki Miss Morogoro 2013 ambapo namkariri akisema “wiki mbili zilizopita nilipata msg kwamba Kidoti hair na Mzinga Planet wanahitaji mamodo kwa ajili ya kutengeneza matangazo kwa ajili ya nywele za kidoti, tulikua Morogoro kwa ajili ya Miss Morogoro tukaja Dar mpaka Mzalendo Pub msg ilipotuelekeza lakini nilivyoingia sikuona mtu ambae anahusiana na Jokate, niliona watu ambao nawajua lakini sio kuhusu nywele’ ‘Nikampigia kaka mmoja anaitwa Johnson kwa sababu najua anafahamiana na Jokate, nikampigia kumfokea kumwambia nyinyi vipi mbona mmetangaza audition alafu sioni hata mtu mmoja ambae anahusika? naona watu ambao kampuni zao zipo majumbani kwao? baada ya dakika zaidi ya 10 kina Jokate wakawa wameshafika japo baadhi ya mamodo wengine walikua wameshaondoka lakini baadhi ya viongozi kama Majaji wa kike walikuepo na walipoulizwa wakasema tumsubiri Mpeka ambae ndio muhusika na pia Mkurugenzi wa Mzinga Planet” – Blessing Baada ya kina Jokate kufika Mpeka alipigiwa simu ili arudi Mzalendo Pub, japo alisita sana mtuhumiwa huyu alikuja kwenye eneo la tukio na kukutana uso kwa uso na Jokate na timu yake, baada ya hapo akaanza kusingizia kwamba yeye hausiki ila kuna watu wengine ndio wanahusika ila alipotoa namba zao wakapigiwa simu, kila mmoja alionekana kutaharuki kwa sababu hawajui chochote kuhusu hiyo Mzinga Planet. Baada ya Jokate na timu yake kukaa na Mpeka na kumuuliza kistaarabu bila kutoa ushirikiano wa kutosha, uamuzi ulitoka kwamba apelekwe Polisi Osterbay ili kuendelea na taratibu nyingine za kisheria. Mpeka alikua anaonekana analia wakati mwingie na hiyo ilikua ni baada ya kumpiga huyu msichana shuhuda aitwae Blessing kwa sababu alimchomea mpaka akakamtwa.
Jokate amesema “miongoni mwa mabinti waliowahi kutapeliwa na matapeli wanaotumia jina la Jokate Mwegelo au Kidoti ni pamoja na mrembo mmoja alipelekwa kwenye hoteli Arusha ambapo mwanaume alimwambia kama atalala nae hotelini atapata fursa ya kuwa model wa Kidoti, alilala nae siku tatu hotelini alafu baadae mwanaume akaondoka ghafla na kuiba simu za huyu mrembo na laptop na hata bili akamwachia yule msichana ndio alipe” Hii audition aliyoifanya Mpeka, usaili mdogo ambao ni Wasichana takribani arobaini walijitokeza, ‘mtu akisikia tangazo kama hili au kama nikiwa na kitu ofcourse watu watakisikia kwenye Amplifaya au millardayo.com na pia niko twitter @JokateM kwa hiyo itakua ni rahisi kutambua kweli kama hiki kitu kimetoka kwa Jokate’
by millardayo.com

Ni French Montana na Jeremih wametusogezea hii video yao mpya

                  

Ile kesi ya kumpiga Rihanna ni kama bado inamtia gundu Chris Brown…

Chris Brown ni kama huu mwaka haujaanza poa kwake, katika vitu ambavyo amekutana navyo ni vikwazo kwenye kazi yake ya muziki. Hapahapa kwenye millardayo.com siku ya January 02 mwaka huu nilikuandikia story ya staa huyo kushindwa kwenda kupiga show yake Ufilipino baada ya kupoteza passport muda mfupi kabla ya safari, wiki chache mbele akashindwa pia kuanza tour yake ya ‘Between the Sheets‘ baada ya Mahakama kumzuia ili amalizie saa 100 za adhabu ya kufanya kazi za kijamii kutokana na kesi ya kumpiga Rihanna ambayo imeendelea kuwepo Mahakamani kwa zaidi ya miaka mitano. Leo kuna story ambayo iko kwenye headlines kuhusu yeye tena, amezuiwa kuingia Canada kufanya show kubwa ambayo ilikuwa ifanyike siku ya leo February 25, sababu haijafahamika lakini ishu ya kesi yake hiyo inatajwa kwamba huenda imemtia doa kutokana na Sheria za nchi nyingi Duniani kutoruhusu mtu ambaye ana rekodi za uhalifu kuingia ndani ya nchi zao.
Chris aliandika kwenye ukurasa wake Twitter kwamba anasikitika kuikosa show hiyo; “The good people of the Canadian government wouldn’t allow me entry. I’ll be back this summer and will hopefully see all my Canadian fans!”—Tweet ambayo muda mfupi baadaye aliifuta. Jamaa ambao waliandaa show hiyo wamesema wanafanya utaratibu ili kupata kibali cha kumruhusu Chris kuingia Canada ili amalizane na ‘deni’ la kutoa burudani kwa fans wake, japo wamesema kwa wale ambao wameshanunua ticket wanaweza kurudishiwa pesa zao kwenye vituo walikouziwa ticket hizo.

Wakati wa maombolezo utaratibu wa hawa ndugu ni kukatwa vidole..

Utamaduni wa watu duniani unatofautiana, moja ya story ambazo sikuwahi kufahamu ni juu ya huu utamaduni wa jamii ya watu wa Dani iliyoko Magharibi mwa Papua, New Guinea ambapo utamaduni wao unahusisha inapotoke msiba wa ndugu yoyote basi ndugu wa marehemu wanaomboleza kwa kujikata vidole. Hii imeshtua wengi walioisikia, kwa wale waliobahatika kuitembelea basi ni mashuhuda kwamba watu wengi wa kutoka jamii hiyo wamekatwa vidole na ndugu yoyote wa marehemu anakatwa vidole, umri sio kitu kinachoangaliwa sana hivyo hata watoto pia wanaguswa na hii moja kwa moja.
Utaratibu huo huwa unakuwa na ibada ya utangulizi ili kufukuza mapepo ya marehemu halafu linafuatia zoezi la kukata vidole, kwa utamaduni huo maumivu ya mwili huonyesha huzuni ya kufiwa pamoja na kuonyesha upendo kwa marehemu. Hapa vidole vinakatwa kwa shoka, vipande vilivyokatwa vinachomwa moto halafu majivu yanahifadhiwa au kuzikwa pamoja na mwili wa marehemu. Jitihada zimeanza kufanywa ili kuzuia utamaduni huo ambao madhara yake yameanza kuonekana kwa sasa
by millardayo.com

HATIMAE BODI YA FILAMU TANZANIA IMEIFUNGIA FILAMU YA FIFTY SHADES OF GREY

Taarifa Kwa Umma Bodi ya Filamu na Michezo ya Kuigiza Tanzania inawaagiza Wamiliki wote wa kumbi za filamu Tanzania Bara kutofanya maonesho ya hadhara ya filamu yenye jina la FIFTY SHADES OF GREY inayoongozwa na Sam Taylor Johnson na kutengenezwa na Michael De Luka, Dana Brunetti na E.L. James.
Hatua hiyo imechukuliwa baada ya Bodi ya Filamu na Michezo ya Kuigiza Tanzania kukagua filamu hiyo yenye urefu wa saa 2:05 na kugundua kwamba haizingatii sheria na kanuni zinazosimamia tasnia ya filamu nchini. Maamuzi haya yamefanywa kulingana na ukiukwaji wa Sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza Na. 4 ya mwaka 1976 kifungu cha 15 (i) na kifungu 18(i na ii) ambayo ufafanuzi wa utekelezaji wake uko katika Kanununi za Sheria hiyo Kifungu cha 24 vifungu vidogo vya a,b,d,e,n na t. Filamu ya FIFTY SHADES OF GREY hairuhusiwi kuonyeshwa popote Tanzania. Aidha, Bodi ya Filamu na Michezo ya Kuigiza Tanzania inawakumbusha kwa mujibu wa Sheria tajwa hapo juu Wamiliki wote wa kumbi za sinema na maeneo yote ya kuonyeshea filamu kuwasilisha filamu katika Bodi hiyo ili zikaguliwe na kupangiwa daraja kabla hazijaanza kuonyeshwa na kutofanya hivyo ni ukiukwaji wa sheria
Pia uzinduzi wowote wa filamu unaofanywa katika kumbi za sinema na maeneo yoyote ya kuonyeshea filamu ni lazima uwe na kibali kutoka Bodi ya Ukaguzi wa Filamu na Michezo ya Kuigiza.

RIYAMA AZUNGUMZIA MAISHA YAKE YA KIMAPENZI

MWIGIZAJI Nyota katika tasnia ya filamu Nchini Riyama Ali amefunguka kwa kusema kuwa upendo wake kwa mpenzi wake ni wa kila siku hauna siku maalum kwani haoni faida ya kuwa na upendo wa kuchaguliwa na mtu hivyo haoni umuhimu wa Valentine Day kwani si mtu wa namna hiyo. “Nampenda laazizi wangu siku zote sioni umuhimu wa mambo ya kuigi ya wazungu eti niwe na siku ya maalum ya kumuonyesha upendo mpenzi wangu siwezi, wala kuvaa nguo za rangi.”anasema Riyama. Riyama anasema kuwa anaamini kuwa siku kama hiyo kwa kuiga inaweza kuwa ni siku ambayo inasababisha mahusiano mapya na kuvunjika kwa mapenzi ya zamani, kwa sababu ya kuiga tamaduni kutoka nje wakati tayari tuna tamaduni zetu, yeye haoni faida ya kuiga vitu ambavyo si utamaduni wa kwake.

WATAKA WANAFUNZI WAFUNDISHWE NGONO MASHULENI

Shule zote za serikali zikiwemo za msingi na zile za upili nchini Uingereza zitalazimika kufunza somo la ngono na uhusiano SRE ,wabunge wa taifa hilo wamesema katika ripoti yao. Kamati ya elimu katika bunge la Uingereza ilianzisha uchunguzi baada ya kubainika kuwa zaidi ya thuluthi moja ya shule zilikuwa zikishindwa kutoa mafunzo ya somo hilo kwa aumri unaohitajika. Mwenyekiti wa kamati hiyo Graham Sturat amesema kuwa vijana wadogo wana haki ya kupata habari ambazo zitahakikisha usalama wao. Serikali imesema kuwa itaangazia matokeo ya ripoti hiyo. Mwaka 2013 ripoti ya bunge hilo ilisema kuwa masomo ya kibinafsi,ya kijamii ,afya na elimu ya kiuchumi ambapo somo hilo la ngono limehusishwa yanahitaji kuimarika katika asilimia 40 ya shule. Wabunge hao wamesema:Hali hii haitakubalika katika masomo mengine licha ya kuwa harakati za serikali kuimarisha masomo hayo ni za kiwango cha chini. Je,unakubaliana na wazo la bunge la Uingereza kuwafunza watoto wa shule za msingi somo la ngono na uhusiano? Kwa maini yako basi ingia katika mtandao wetu wa faceboo katika bbcswahili.

BAADA YA KUFANYA MAKOSA AAMUA KUYATUNGIA KITABU

Baada ya kugundua amefanya makosa tofauti tofauti Aliyekuwa mke wa rapa Wiz Khalifa ‘Amber Rose’ ametangaza ujio wa kitabu chake kuhusu makosa aliyofanya kwenye maisha yake mpaka kupelekea yeye kuwa kama alivyo. Kitabu kitaitwa “How To Be a Bad B*tch” na kinategemewa kutoka November 2015. Kitabu kitachapishwa na kampuni ya Simon & Schuster. Kuna uvumi kuwa Kim Kardashian amemuomba dada yake ‘Khloe’ amalize beef yao na Amber sababu Amber ana siri nyingi za Kanye West.