Ile kesi ya kumpiga Rihanna ni kama bado inamtia gundu Chris Brown…
Chris Brown ni kama huu mwaka haujaanza poa kwake, katika vitu ambavyo amekutana navyo ni vikwazo kwenye kazi yake ya muziki.
Hapahapa kwenye millardayo.com siku ya January 02 mwaka huu nilikuandikia story ya staa huyo kushindwa kwenda kupiga show yake Ufilipino baada ya kupoteza passport muda mfupi kabla ya safari, wiki chache mbele akashindwa pia kuanza tour yake ya ‘Between the Sheets‘ baada ya Mahakama kumzuia ili amalizie saa 100 za adhabu ya kufanya kazi za kijamii kutokana na kesi ya kumpiga Rihanna ambayo imeendelea kuwepo Mahakamani kwa zaidi ya miaka mitano.
Leo kuna story ambayo iko kwenye headlines kuhusu yeye tena, amezuiwa kuingia Canada kufanya show kubwa ambayo ilikuwa ifanyike siku ya leo February 25, sababu haijafahamika lakini ishu ya kesi yake hiyo inatajwa kwamba huenda imemtia doa kutokana na Sheria za nchi nyingi Duniani kutoruhusu mtu ambaye ana rekodi za uhalifu kuingia ndani ya nchi zao.
Chris aliandika kwenye ukurasa wake Twitter kwamba anasikitika kuikosa show hiyo; “The good people of the Canadian government wouldn’t allow me entry. I’ll be back this summer and will hopefully see all my Canadian fans!”—Tweet ambayo muda mfupi baadaye aliifuta.
Jamaa ambao waliandaa show hiyo wamesema wanafanya utaratibu ili kupata kibali cha kumruhusu Chris kuingia Canada ili amalizane na ‘deni’ la kutoa burudani kwa fans wake, japo wamesema kwa wale ambao wameshanunua ticket wanaweza kurudishiwa pesa zao kwenye vituo walikouziwa ticket hizo.
Related Post:
Tanzia: Muongozaji wa filamu na vipindi vya TV George Tyson Afariki kwa ajali ya gari Msiba mkubwa umeikumba tasnia ya filamu na habari Tanzania, George Tyson muongozaji mkongwe wa … Read More
AUDIO: YALIYOJILI KATIKA MAZIKO YA MSANII ADAM KUAMBIANA Waziri wa Habari vijana Utamaduni na Michezo, Dkt. Fennella Mukangara, akitoa heshima… Read More
Audio: DJ Choka ailezea ajali ya gari alilokuwemo George Tyson na hali ya waliokuwa kwenye gari hilo Jana usiku wadau wa filamu na vipindi vya TV walipatwa na mshituko baada ya kupata taarifa k… Read More
ZITTO KABWE AJIBU TUHUMA JUU YA KUNDI LA KIGOMA ALL STAR'S Jana mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi ambaye ni msemaji wa kambi ya upinzani kuhusu Habari,… Read More
Brad Pitt apigwa na 'ripota' kwenye uzinduzi wa filamu mpya ya Angelina Jolie Muigizaji Brad Pitt alijikuta katika wakati mgumu Jumanne iliyopita katika uzinduzi wa filam… Read More
Posted by Unknown
on Wednesday, February 25, 2015,
Add Comment
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Response to "Ile kesi ya kumpiga Rihanna ni kama bado inamtia gundu Chris Brown…"
Post a Comment