Latest Updates

RIYAMA AZUNGUMZIA MAISHA YAKE YA KIMAPENZI

MWIGIZAJI Nyota katika tasnia ya filamu Nchini Riyama Ali amefunguka kwa kusema kuwa upendo wake kwa mpenzi wake ni wa kila siku hauna siku maalum kwani haoni faida ya kuwa na upendo wa kuchaguliwa na mtu hivyo haoni umuhimu wa Valentine Day kwani si mtu wa namna hiyo. “Nampenda laazizi wangu siku zote sioni umuhimu wa mambo ya kuigi ya wazungu eti niwe na siku ya maalum ya kumuonyesha upendo mpenzi wangu siwezi, wala kuvaa nguo za rangi.”anasema Riyama. Riyama anasema kuwa anaamini kuwa siku kama hiyo kwa kuiga inaweza kuwa ni siku ambayo inasababisha mahusiano mapya na kuvunjika kwa mapenzi ya zamani, kwa sababu ya kuiga tamaduni kutoka nje wakati tayari tuna tamaduni zetu, yeye haoni faida ya kuiga vitu ambavyo si utamaduni wa kwake.

0 Response to "RIYAMA AZUNGUMZIA MAISHA YAKE YA KIMAPENZI"

Post a Comment