Latest Updates

HATIMAE BODI YA FILAMU TANZANIA IMEIFUNGIA FILAMU YA FIFTY SHADES OF GREY

Taarifa Kwa Umma Bodi ya Filamu na Michezo ya Kuigiza Tanzania inawaagiza Wamiliki wote wa kumbi za filamu Tanzania Bara kutofanya maonesho ya hadhara ya filamu yenye jina la FIFTY SHADES OF GREY inayoongozwa na Sam Taylor Johnson na kutengenezwa na Michael De Luka, Dana Brunetti na E.L. James.
Hatua hiyo imechukuliwa baada ya Bodi ya Filamu na Michezo ya Kuigiza Tanzania kukagua filamu hiyo yenye urefu wa saa 2:05 na kugundua kwamba haizingatii sheria na kanuni zinazosimamia tasnia ya filamu nchini. Maamuzi haya yamefanywa kulingana na ukiukwaji wa Sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza Na. 4 ya mwaka 1976 kifungu cha 15 (i) na kifungu 18(i na ii) ambayo ufafanuzi wa utekelezaji wake uko katika Kanununi za Sheria hiyo Kifungu cha 24 vifungu vidogo vya a,b,d,e,n na t. Filamu ya FIFTY SHADES OF GREY hairuhusiwi kuonyeshwa popote Tanzania. Aidha, Bodi ya Filamu na Michezo ya Kuigiza Tanzania inawakumbusha kwa mujibu wa Sheria tajwa hapo juu Wamiliki wote wa kumbi za sinema na maeneo yote ya kuonyeshea filamu kuwasilisha filamu katika Bodi hiyo ili zikaguliwe na kupangiwa daraja kabla hazijaanza kuonyeshwa na kutofanya hivyo ni ukiukwaji wa sheria
Pia uzinduzi wowote wa filamu unaofanywa katika kumbi za sinema na maeneo yoyote ya kuonyeshea filamu ni lazima uwe na kibali kutoka Bodi ya Ukaguzi wa Filamu na Michezo ya Kuigiza.

0 Response to "HATIMAE BODI YA FILAMU TANZANIA IMEIFUNGIA FILAMU YA FIFTY SHADES OF GREY "

Post a Comment