MAHAKAMA YAAMURU FAMILIA YA MARVIN GAYE KULIPWA FIDIA
Mahakama nchini Marekani imetoa uamuzi kuwa mwandishi wa wimbo wa Blurred lines, ambayo ni singo iliyouza mno, aliiba mashairi ya wimbo wa Marvin Gaye.
Jopo la wazee wa mahakama Jijini Los Angeles limesema singo hiyo ya mwaka 2013 iliyoimbwa na Pharrell Williams na Robin Thicke imevunja sheria za hati miliki kwa kuiba mashairi ya wimbo Got To Give It Up wa Gaye alioutoa mwaka 1977.
Kutokana na kosa hilo mahakama imeamuru familiya ya marehemu Mravin Gaye, kulipwa dola milioni 7.3 kama fidia.
Hata hivyo Thicke na Williams wamekanusha kuiga traki hiyo kali na wakili wao amesema uamuzi huo wa mahakama ni wa kutisha
by Zourha Malisa
Posted by Unknown
on Monday, March 16, 2015,
Add Comment
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Response to " MAHAKAMA YAAMURU FAMILIA YA MARVIN GAYE KULIPWA FIDIA"
Post a Comment