Majibu ya msanii TID baada ya kuulizwa kuhusu Q Chief
tid4Akiwa kwenye kipindi cha XXL msanii TID aliulizwa kinachoendelea kati yake na msanii Q Chief kutokana na maneno aliyoyazungumza juu yake hivi karibuni, TID amesema kuwa hamsikii Q Chief hata akiongea hamsikii.
TID amesema kuwa hataki kuzungumzia suala hilo kwa sababu Q Chief akisikia ndio atataka kuzungumza zaidi na yeye hataki kuyazungumzia kwa kuwa yameshapita.
Ishu ya kumsimamia msanii Abulnas amesema kwa sasa kazi inaenda vizuri, anatarajia kufanya ngoma yake ya pili na msanii Wyre kutoka Kenya na tayari ameshatumiwa beat lakini hawatoiachia.
TID amesema akimuangalia msanii huyo anakumbuka maisha ya rafiki yake Albert Mangwea ingawa hawezi kuziba pengo lake lakini ni rafiki ambaye yuko nae muda wote.
Posted by Unknown
on Friday, February 20, 2015,
Add Comment
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Response to "Majibu ya msanii TID baada ya kuulizwa kuhusu Q Chief"
Post a Comment