Latest Updates

Maneno ya Sajna kuhusu Bangi na kuondoka Tetemesha Records..

Najua haujasahau watu waliokuwa wakitajwa sana kwenye chati ya Bongo Fleva akiwemo msanii Sajna ambaye ukimya wake unaambatana na story nyingi sana, mengine yamesemwa kuwa ni stress za kazi mpaka kujihusisha na matumizi ya bangi na pombe. Sasa time hii amemplify na kuyajibu yale yaliyozungumzwa na kusema; “Kwa sababu muziki unahitaji msimamizi na ukikosa msimamizi hauwezi kufanya kitu chochote na pia watu wanajua kwamba huyu msanii ni anasimamiwa na fulani, wengi hawajui kwamba mimi nimeachana na Kid Bway wanajua kwamba mimi nipo na Kid Bway lakini kuna matatizo tu yalitokea ndio maana nakaa kimya sana ila najipanga upya niweze kurudi Tetemesha“ Ripota wa nguvu:“Sababu kubwa hasa ya kuachana na Kid Bway ni nini?…“ Sajna: “Ni matatizo tu ya kikazi kidogo kidogo siwezi kuyaongelea ni kawaida tu inatokea kwenye kazi ,sasa hivi inakimbilia mwaka kama sio mwaka basi inakimbia miezi tisa tangu niachane na Kid bway, meneja wangu alikuwa anasimamia muziki alikuwa anajua mapungufu yangu, kweli kuna wakati mwingine siwezi kufanya muziki Kid ila nahitaji kurudi Tetemesha lakini basi siwezi kuongea mengi“ Ripota wa nguvu: “Kuna tetesi za wewe kutumia bangi, pombe hili unalizungumziaje?…“ Sajna…”Unajua ukiwa msanii kila mtu anazungumza la kwake unaweza ukaambiwa fulani ana ukimwi labda hivi na hivi, kama mtu anataka kuamini mimi navuta banga mpaka uhakikishe sema watu wakinikuta maeoneo fulani ndio kila mtu anazungumza lakini sio kwamba mimi navuta bangi, lakini pombe natumia bia mbili, tatu bangi hata ukoo wetu hawatumia..“

0 Response to "Maneno ya Sajna kuhusu Bangi na kuondoka Tetemesha Records.."

Post a Comment