Latest Updates

WEMA ATOA KALI YA KUMALIZIA MWAKA

                      
Ile Nissan Murano alilozawadiwa  Wema Sepetu na aliyekuwa mpenzi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’, limeanza kumchefua mrembo huyo kiasi cha kulisusa.

Tukio hilo lilijidhihirisha wazi nyumbani kwa wema,Kijitonyama jijini Dar, ambapo Wema alitamka hadharani kuwa kwa sasa analichukia kupita maelezo gari hilo alilozawadiwa na Diamond kwenye sherehe yake ya kuzaliwa.
                     
“Bwana acha nitumie hili gari lingine kwenda Airport hilo Murano sitaki hata kulisikia, sijui najisikiaje hata nikiliona,” alisikika Wema. Wema akionesha wazi kuwa analichukia gari hilo, alimuuliza sababu inayomfanya alichukie ambapo alisema hajui ni kwa nini analichukia ingawa ni mali yake.

“Siku hizi sipendi kutumia hili Murano tena nalichukia kweli, inafikia kipindi nakosa raha nikiliona lakini ukiniuliza sababu ya kulichukia kiasi hicho hata sina sijui nimezoea sana kutumia BMW, ndiyo maana najikuta nalichukia gari hili,” alisema Wema.
                  
Kwenye bethidei yake iliyofanyika Septemba, mwaka huu, Wema alizawadiwa magari mawili. La kwanza lilikuwa ni BMW 545i  ambalo liliibua utata juu ya mtu aliyemzawadia na la pili ni Nissan Murano alilopewa na Diamond

0 Response to " WEMA ATOA KALI YA KUMALIZIA MWAKA "

Post a Comment