Latest Updates

Dr. Dre katoa zawadi ya Christmas kwa timu yake,


Dr-Dre-December-2014-BellaNaija0031Zawadi.. Zawadi.. Zawadi…
Sikukuu ya Christmas haiko mbali sana, wapo wanaotoa zawadi na wapo wanaopokea pia katika kipindi hiki.
Tajiri, Rapper mkongwe kutoka Marekani ambaye ni juzi tu Dunia nzima imeambiwa na jarida la Forbes kwamba kile kiasi cha pesa alichozalisha Hiphop Mogul huyo kimemfanya namba moja, sio Marekani bali Duniani, sio kupitia show za muziki ila ‘Beats by Dre’ ikidhihirisha kwamba ni biashara nzuri kwa upande wake.
Dr. Dre ametoa zawadi kibao, hazijatajwa lakini juu ya zawadi hiyo kuna fungu la kama dola 10,000 kwa kila mtu ambaye ni mfanyakazi wa kampuni ambayo inasimamia masuala yake ya Kisheria.
Sio wanasheria na wasaidizi wao, unaambiwa zawadi hii imemkuta kila mtu ndani ya kampuni hiyo.
Dre WSJ
Hiyo ni bonus kwa kazi yao nzuri, bado hana hasara.
Umetoa ama kupokea zawadi yoyote Christmas hii?
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza

0 Response to " Dr. Dre katoa zawadi ya Christmas kwa timu yake,"

Post a Comment