Latest Updates

Utaishangaa hii ya kijana aliyefanya upasuaji ili afanane na Kim Kadarshian…


kim4Kijana mwenye miaka 23 Jordan James Uingereza ameripotiwa kutumia paundi 100,000 sawa na zaidi ya milioni 160 za kitanzania ili afanyiwe upasuaji na kufanana kama mwanamitindo Kim Kadarshian.
Safari yake ya kutaka kujibadilisha ilianza baada ya kumuona Kim Kadarshian katika Tv shoo inayorushwa na kituo cha E news inayojulikana kama Keep Up with Kardashians miaka michache iliyopita  na kuvutiwa na mwanamitindo hiyo maeneo mbalimbali ya mwili wake ikiwemo macho,mdomo pamoja na sura yake na kutamani kuwa kama yeye.
kim5
Mbali na hilo pia aliripotiwa kutumia kiasi kikubwa cha pesa kununua vitu vya thamani ikiwemo mavazi anavyomiliki Kim Kardashian ambavyo hutengenezwa na makampuni makubwa ya Prada,Louis Vuitton,Channel na mengine ili mradi aweze kuonekana kama yeye,
Akizungumzia sababu za kutaka afanane na staa huyo ambaye ni mke wa rapa Kanye West alifafanua kuwa “huwa navutiwa na midomo ya dada huyu na sehemu mbalimbali za mwili wake,nilicheka sana siku niliposikia watu wananitukanakwa nini nimeamua kufanya upasuaji nakuonekana feki,wanadhani mimi nafanya ili nionekana wa kawaida? kama ingekua hivyo ningewaambia madaktari warudishe pesa zangu,”alisema.
kim3
Alisema bado hajamaliza matakwa yake na sasa anafikiria kubadilisha pua yake ifanane na mwanamitindo huyo na endapo ataishiwa fedha za kufanya mabadilio hayo yupo tayari kuazima hata kwa familia yake.
“Muonekano wangu mpya kwa watu unanifanya nijisikie fahari kubwa..napenda watu wanavyotumia muda wao kunitazama,kwa wale wote ambao hawapendi muonekano wangu wajue kuna wengine wanapenda.wajue ndio watu pekee ninaowajali pia”alisema.
kim2
Ameongeza kuwa Kim Kardashian amekua mtu pekee anayevutiwa nae duniani kote na huwa anaheshimu na kuthamini kazi zake na ndio maana ameweza kutumia muda na fedha zake kutaka kuudhihirishia Ulimwenguni jinsi gani anamkubali.

0 Response to " Utaishangaa hii ya kijana aliyefanya upasuaji ili afanane na Kim Kadarshian…"

Post a Comment