Latest Updates

Ni zamu ya Madonna 2015…hii inahusu ziara yake kuzunguka dunia nzima


madonnn 
Mwanamuziki Madonna Louise ni miongoni mwa mastaa barani Ulaya wanaofanya vizuri katika kazi zao za kimuziki na kujikuta akitumia taaluma yake vyema katika kujiongezea kipato.
Tayari mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 56 amejiwekea malengo ya kufanya ziara ya kuzunguka dunia nzima mwakani jambo ambalo hakuwahi kulifanya katika maisha yake ya muzuki.
Sababu kubwa ya kufanya hivyo ni pamoja na kusherehekea kutimiza miaka 30 kwa albamu yake ya ‘Like a Virgin’ aliyoitengeneza mwaka 1985 na sasa inatimiza miaka 30 kwa mafanikio makubwa sambamba na maandalizi ya albamu nyingine mpya.
“Hii itakua tuu muhimu sana na ya aina yake,Madona anatamani kuhakikisha albamu yake itakayotimiza miaka 30 inaonekana duniani kote”
Alisma kama alivyofanya katika ziara ya albamu yake ya MDNA katika nchi za Afrika Kusini,Ulaya na Asia sasa atatamani kuona albam hii inawafikia watu wote dunia wakati akifanya ziara hiyo.
Mpaka sasa tayari ana ziara nane ambazo anatakiwa kuzifanya na amejipanga kuhakikisha mwakani anatimiza malengo yake muhimu katika doto alizojiwekea.

0 Response to " Ni zamu ya Madonna 2015…hii inahusu ziara yake kuzunguka dunia nzima"

Post a Comment