Latest Updates

Story za alichosema Baba wa Beyonce kuhusu kufilisika…Picha nyingine za Jay Z na Beyonce Thailand

Kulikuwa na story mitandaoni ambazo hazikuwa nzuri kwa familia ya mzee Mathew Knowles,
ikasemekana eti amefilisika mpaka kafikia hatua ya kuuza vitu
mbalimbali ikiwemo nguo za mtoto wake, yaani Beyonce pamoja na CD za
nyimbo.
Hii haikuwa taarifa nzuri, Beyonce kaongoza kwa kuingiza pesa nyingi upande wa mastaa wa kike Marekani, ina maana amemtelekeza Baba yake kiasi hicho?
Mzee Knowles amekanusha story hizo; “Ningehitaji pesa nisingeuza T-shirt ya dola 5, ningeuza tuzo ya Grammy au BET…

Mzee huyo kasema anauza vitu hivyo ili
kupunguza mlundikano wa vitu ambavyo vilikuwa vinajaza nafasi tu ndani
ya jengo la ofisi yake ambayo anapanga kuikarabati upya mwaka 2015.
Kwa hesabu ya haraka haraka ya vitu anavyoviuza Mzee Knowles ni kama atapata dola 2000/= tu.
Hayo yanaendelea Marekani, lakini Beyonce yuko na familia yake, Jay Z na mtoto wao Blue Ivy maeneo ya Thailand, picha za mwisho wameshare wakiwa kwenye ukumbi mkubwa wa Michezo wa  Muay Thai wakiangalia mchezo wa ngumi.


                                                                       millardayo
               

0 Response to "Story za alichosema Baba wa Beyonce kuhusu kufilisika…Picha nyingine za Jay Z na Beyonce Thailand"

Post a Comment