Latest Updates

Hii ni furaha nyingine kwa familia ya mwanamuziki Alicia keys na Swizz Beatz…

Safari hii ni zamu ya familia ya mastaa wawili wa Marekani, Alicia keys na mume wake ambaye ni producer mkali, Swizz Beatz kupata mtoto usiku wa Dec 27 na kuifanya siku hiyo kuwa ya furaha kwa kuongeza mwanafamilia. Mtoto wa mastaa hao ni wa kiume aliyepewa jina la Genesis Ali Dean, huyu ni pili wa kwanza ni Egypt Daoud, waliompata miaka minne iliyopita. Alicia alielezea furaha yake kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kushare kadi yenye iliyoonyesha kuzaliwa mtoto wake na kuandika. “The joy of joy is joy!! It’s a boy… We are so grateful!! #blessings!!”– @aliciakeys

0 Response to "Hii ni furaha nyingine kwa familia ya mwanamuziki Alicia keys na Swizz Beatz…"

Post a Comment