Latest Updates

Mshindi wa Miss Universe 2014 hatoiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya dunia, sababu iko hapa

Kamati ya Miss Universe Tanzania imemteua mshindi wa pili wa Miss Universe 2014, Nale Boniface kwenda kuiwakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa ya Miss Universe yatakayofanyika mwanzoni mwa mwezi wa kwanza 2015 Miami, Marekani. Taarifa rasmi inasema hatua hii imechukuliwa baada ya mshindi husika Miss Universe Tanzania 2014 Carolyne Bernard kupata ajali na kuvunjika kidole chake cha mguu. Ripoti ya daktari imeonesha kuwa kupona kwake kutachukua mwezi mmoja wakati mrembo anatakiwa awe mashindanoni baada ya siku kumi kuanzia sasa na isitoshe awapo mashindanoni mrembo atapaswa kuvaa viatu virefu (High heels) wakati wote ambapo haishauriwi kiafya kutokana na tatizo lake. Kutokana na hali hii, Nale Boniface ambaye alishika nafasi ya pili na kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss Earth ndiye atakayekwenda kuiwakilisha nchi badala yake kama mkataba unavyoainisha na hivyo atakuwa Miss Universe Tanzania 2014. Kamati inasikitishwa na kuumia kwa Carolyne na inaahidi kuendelea kuwa nae bega kwa bega katika matibabu yake kwani bado yupo chini ya mkataba wa Miss Universe Tanzania kwa mwaka mzima. Mashindano ya Miss Universe Tanzania mwaka huu yalifanyika tarehe 31 mwezi wa kumi.

0 Response to "Mshindi wa Miss Universe 2014 hatoiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya dunia, sababu iko hapa"

Post a Comment