Latest Updates

Majambazi walivamia kanisani wakaiba pesa za Kanisa, kilichofuatia ni hiki…

Kuna mambo yakitokea unajikuta unajipima na kuitazama imani yako iko kwa kiasi gani? Tumezoea matukio mengi ya kihalifu hujitokeza wakati wa sikukuu, ujambazi, wizi na uhalifu mwingine. Hawa jamaa waliingia kanisani St. Petersburg, Russia wakaiba pesa ambazo kiwango chake hakijafahamika wakaingia kwenye gari na kuanza kukimbia, Polisi wakaanza kuwafukuza lakini safari yao haikuishia mbali. Gari ya jamaa hao ilipigwa shoti ya umeme, gari ikashika moto, waliokuwemo ndani wote hakuna aliyeweza kutoka mzima hata mmoja. Gari nyingine iliyokuwa pembeni yake iliathirika kiasi kidogo kutokana na shoti hiyo lakini hakuna mtu aliyedhurika. Video hii ya dakika 2 ilirekodiwa na camera iliyofungwa kwenye gari ya polisi, inaonyesha tukio zima lilivyokuwa.

0 Response to "Majambazi walivamia kanisani wakaiba pesa za Kanisa, kilichofuatia ni hiki…"

Post a Comment