Latest Updates

Maamuzi ya Rais Kikwete kuhusu maazimio ya Bunge, kuwawajibisha Mawaziri na akaunti ya Tegeta Escrow

Rais Kikwete leo December 22 amehutubia Taifa kwa kufanya mazungumzo na wazee wa Dar es Salaam ambapo amezungumzia mambo makuu mawili; kwanza kuhusu Uchaguzi Serikali za Mitaa na pia maazimio ya Bunge kuhusu uchotwaji wa pesa kwenye akaunti ya Tegeta Escrow. Kuhusiana na maamuzi yaliyotolewa na Waziri Hawa Ghasia kwa Wakurugenzi ambao hawakuwajibika kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Rais Kikwete amesema; “Katika taarifa ya waziri Ghasia alielezea kasoro zilizojitokeza na aliahidi kuchukua hatua. Nieleze furaha yangu kwa Hawa Ghasia juu ya hatua alizochukua na mimi nikaweka ridhaa yangu… “ Rais Kikwete alitolea ufafanuzi wa uhalali wa fedha za Escrow kuwa mali ya umma ama mali ya IPTL; “…Maelezo haya kwa kiasi fulani yanasaidia kwenye kupata jibu la swali maarufu, fedha hizi hasa mwenyewe nani? Akaunti ya Escrow ni akaunti maalum inayoanzishwa kwa ajili ya sababu maalum, kufanya kazi maalum, kwa masharti maalum na kazi hiyo ikiisha na akaunti yenyewe inafungwa… Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali akasema aaah.. nyinyi si mliletewa madai? Si mmelipa? Hata kama hazijaenda kwa mwenyewe msizihesabu kuwa ni zenu, hizi sio zenu…” “Fedha zilizowekwa kwenye akaunti ya Escrow hazina sifa ya kutafsiriwa kama ni mali ya TANESCo, hivyo marekebisho yamefanywa ili kutotambua mali na madeni yanayohusu fedha hizo kwa kiasi cha fedha zilizopo kwenye akaunti ya Escrow… Ni dhahiri kwamba fedha zilizokuwa kwenye akaunti ya Escrow sio za TANESCo na hazikupaswa kuingizwa kwenye vitabu vya TANESCo kama mali yake… Kama si za TANESCo ni za IPTL…“ Bodi ya TANESCo iliyopo sasa imemaliza muda wake tumeanza mchakato wa Bodi mpya… Katibu Mkuu wa Wizara tumejadili hili katika Serikali tukasema huyu ni Mtumishi wa Umma.. nimeagiza mamlaka zinazohusika na mchakato huu wazichunguze tuhuma zinazohusika ili kama itadhihiri basi awajibishwe inavyostahiki…“ “... Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameshajiuzulu… Waziri wa Ardhi kupokea fedha kutoka VIP Engineering & Marketing, mazungumzo yetu sana yalikuwa pesa hizi ni za nini, amezipata vipi, kwa ajili gani? Ameeleza kuwa pesa ni za shule… maswali makubwa ambayo yametia shaka sana nakuleta mjadala mkubwa ni kwanini pesa hizi hazikwenda moja kwa moja kwenye shule zikawa kwa jina lake… Tulikubaliana kwamba Waziri huyu na tulikwishazungumza naye kwamba atupe nafasi tumteue mwingine…“– Rais Kikwete. story by Millard Ayo

0 Response to "Maamuzi ya Rais Kikwete kuhusu maazimio ya Bunge, kuwawajibisha Mawaziri na akaunti ya Tegeta Escrow"

Post a Comment