Latest Updates

Hili ni dili analofungia mwaka 2014 msanii Davido…

Mwezi December ni mwezi ambao watu huwa wanafanya uchambuzi wa namna mwaka ulivyokwenda, kuangalia malengo ambayo umeyaweka yamepita au yamekwama na pia kuandaa mikakati mipya ya mwaka unaofuatia. Davido ni mmoja ya mastaa wanaomaliza vizuri 2014, amefanya vizuri kwenye muziki, siku ya December 27 alitoka na tuzo mbili kwenye AFRIMA Awards 2014, msanii Bora wa Mwaka na pia Hit Single yake ya ‘Aye’ kuwa wimbo bora wa mwaka. “JUST SIGNED A DEAL WITH CLOSE UP! GREAT WAY TO END THE YEAR!! NON STOP THANK YOU LORD!! #owonikoko”– @davidoofficial Hizo ni dalili njema kwa Davido 2015, tayari amesign dili ya kutangaza dawa ya mswaki ya Close Up, kasema ina mavuno ya Naira nyingi hivyo mbali na mauzo ya album aliyopanga kuitoa mwakani pamoja na deal nyingine ikiwemo ya shows, kupitia hii kajihakikishia mkwanja wa kutosha 2015.

0 Response to "Hili ni dili analofungia mwaka 2014 msanii Davido…"

Post a Comment