Latest Updates

OBAMA FILAMU YA KIM JONG UN IONYESHWE

Rais wa marekani Barack Obama ameimbia Korea Kaskazini kuwa Marekani itajibu kisa ambapo wizi wa mtandao ulioendeshwa dhidi kampuni ya filamu ya Sony Pictures hali iliyosababisha kufutiliwa mbali kwa maonyesho ya filamu inayomdhihaki kiongozi wa korea kaskazini kim jong- un. Lakini mwandishi wa BBC anasema kuwa hatua hiyo haitakuwa rahisi kwa Marekani kutokana na kujitenga kwa Korea kaskazini. Filamu ya Kumdhihaki Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong Un iliozuiliwa na kampuni ya Sony Pictures kufuatia vitisho Rais Obama amesema kuwa kampnui ya filamu ya Sony Pictures ilifanya makosa kwa kusitisha kuonyesha filamu hiyo. Hata hivyo Sony ilisema kuwa ilichukua uamuzi huo kwa kuwa kumbi nyingi kubwa za sinema nchini Marekani zilikataa kuonyesha filamu hiyo. Sony imesema kuwa ina mipango wa kuionyesha filamu hiyo na kwa sasa inatafuta njia zingine za kuionyesha. KWA HISANI YA BBC.

0 Response to "OBAMA FILAMU YA KIM JONG UN IONYESHWE "

Post a Comment