Latest Updates

AKIMBIA DAR ES SALAAM KISA AOGOPA KUPORWA MPENZI WAKE

MWIGIZAJI wa kike wa filamu katika tasnia ya filamu Loveness Watson ametoa kali pale alipofunguka kuwa ameamua kuhama jiji la Dar es salaam baada ya kuhisi wasanii wenzie wa kike watampora mpenzi wake kama walivyowahi kumpora mwingine.
Zamani walipokuwa wakisema abiria chunga mzigo wako nilikuwa sielewi, lakini sasa najua ukiwa na boyfriend tu ukimchekea shoga yako tu anachukua, sasa nihamia naye Morogoroo mtu akinifuata huku mgomvi nalinda penzi langu,”anasema Love.
Msanii huyo anadai kuwa siku za nyuma rafiki yake kipenzi alimnyanganya mpenzi wake pamoja na kuwa alikuwa ni mtu aliyemsaidia na kumwingiza katika sanaa na yeye akaanza kuonekana kama mwigizaji wa maana lakini siku ya siku shukrani yake alimfanyia unyama, hivyo kahamia Morogoro kwa usalama wa mpenzi wake.

0 Response to " AKIMBIA DAR ES SALAAM KISA AOGOPA KUPORWA MPENZI WAKE"

Post a Comment