Latest Updates

Slim Thugs Amtukana Kobe BryantRappa ambae aliwahi fanya vizuri kupitia wimbo wa check on it alioshirikishwa na Beyonce Knowles amezusha tafrani kupitia mtandao wa twitter baada ya kumtukana mchezaji wa timu ya kikapu ya L.A lakers kobe Bryant
 Rappa  huyo ambae alionekana waz kumchukia mcheza kikapu huyo alianza kutweet mfululizo akianzia katika tukio la kupigwa kiwikio kwa mchezaji huyo kobe Bryant na mchezaji mwenzie wa zamani Dwight howard
Msimu uliopita wa nba Dwight alikua akichezea L.A  lakers na ilidaiwa kua alikua hana  na mahusiano mazuri na mchezaji huyo kobe Bryant
 Katika mfululizo wa tweets hizo Slim thugs aliendelea kumshambulia kwa maneno akisema kua Kobe ni Jordan fake huku katika tweet nyingine akisema wazi kua kobe anaiga mpaka tabia ya kung’ata ulimi ya Michael Jordan
Haijafahamika hasa nini sababu ya chuki za wazi kutoka kwa rapa huyo mtanashati

0 Response to "Slim Thugs Amtukana Kobe Bryant"

Post a Comment