Latest Updates

ROSE AUMIA KUANDIKWA AMEBAKWA


Msanii wa filamu nchini Rose Ndauka ameweka wazi kuwa kitendo kilichowahi kumsikitisha katika maisha yake ni kuandikwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari jambo ambalo halina uwakika na halijathibitishwa na yeye mwenyewe.

Ambapo aliweka wazi kuwa jambo ambalo limemuumiza na hatolisahau ni kuandikwa na moja ya gazeti hapa nchini jambo ambalo kwake anaona si la kawaida.

"Nimeandikwa nimekunywa nimelewa kisha nikabakwa na wanaume zaidi ya watatu, jambo hilo liliniumiza sana na ni jambo ambalo sitoweza kulisahau katika maisha yangu kwani ni kitu ambacho nakikumbuka kila siku" alisema Rose.

Aliongezea kuwa ni vyema waandishi wakatafuta story za ukweli na kuwauliza wausika.

0 Response to "ROSE AUMIA KUANDIKWA AMEBAKWA"

Post a Comment