Latest Updates

Chid Benz arudishwa rumande kwa kushindwa masharti ya dhamana Milioni 1,kesi yake kutajwa Nov 11 MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Chid Benz mchana huu amesimamishwa kizimbani kwa mara ya kwanza   katika mahakama ya Kisutu na kusomewa mashtaka matatu ikiwemo ya Kukutwa na madawa ya kulevya aina ya Heroin yenye thamani ya sh. 38,638 bangi ya sh. 1,720 na vifaa vya kutayarishaji uvutaji wa madawa, ambapo kosa la pili ni Kusafirisha madawa ya kulevya na Utumiaji wa madawa ya kulevya.
Alisomewa mashtaka hayo mbele ya hakimu Mkazi Mkuu Warialwande Lema aliyepangiwa kusikiliza kesi hiyo.
Hata hivyo msanii huyo aliamuriwa kutolewa nje amri hiyo ilitolewa na hakimu baada ya suruali aliyovaa kuonekana kuvaa mlegezo maarufu kama kata kei kuonesha sehemu kubwa ya nguo yake ya ndani.
Mchana wa saa 7 alirejeshwa ndani ya chumba cha mahakama ambapo upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mwanaamina Kombakono akisaidiana na Inspekta Jackson Chidunda ulimsomea mashtaka yake.
Mshtakiwa alikana mashtaka yote na upande wa jamhuri ulidai kuwa hauna pingamizi na dhamana dhidi ya mshtakiwa.
Hakimu Lema aliiweka wazi dhamana hiyo na kutaja masharti ya dhamani ikiwemo kuwa na wadhamini wawili wanaotoka kwenye taasisi zinazoaminiwa na siyo walimu na dhamana ya sh. Milioni moja.
Mshtakiwa alishindwa kutimiza mashrti hayo na amepelekwa mahabusu hadi Novemba 11 kesi hiyo itakapotajwa tena.
Chidi Benz amerudishwa rumande hadi Novemba 11 ambapo atapandishwa tena kizimbani.Dhamana itakuwa wazi kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili wanaoeleweka na pesa taslimu milioni 1.
Credit:Edwin & Zourha

0 Response to " "

Post a Comment