Latest Updates

LULU AHIFADHI NGUVU ZAKE KWA AJILI YA KUJIANDAA KUJIFUNGUA


MASTAA wana mambo! Mtoto mzuri Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ametoa kali ya aina yake kwa kusema kamwe hatumii nguvu nyingi kwenye mapenzi kwa sababu yanapoteza muda bila sababu za msingi bora nguvu zake azitunze hadi pale atakapokuwa akijifungua.

Akimwaga cheche mbele ya mwanahabari wetu, Lulu alisema siku hizi wanaume wengi wanawafanya wasichana watumie nguvu kutetea penzi kutokana na migogoro isiyokuwa na msingi. 

“Bora nguvu zangu nizihifadhi za kuendea leba kuliko kuzipoteza katika mapenzi kwani hayo mambo yamepitwa na wakati kabisa,” alisema Lulu.

0 Response to "LULU AHIFADHI NGUVU ZAKE KWA AJILI YA KUJIANDAA KUJIFUNGUA"

Post a Comment