Latest Updates

NDOA YA SHILOLE NA NUHU NI NDOTO NZITO


IMEBAINIKA kuwa uhusiano wa staa wa Mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, na mpenziwe Nuh Mziwanda ni kazi bure kwani uwezekano wa kufunga ndoa kati yao haupo kutokana na kupishana imani.Ishu hiyo imejidhihirisha juzikati nyumbani kwa wawili hao Mwananyamala-Manjunju jijini Dar, baada ya paparazi wetu kuwaibukia na kutaka kujua malengo yao zaidi kama wana mpango wa kuoana au la, Nuhu alizungumzia uhusiano wao.

“Mimi ninampenda Shilole kwa asilimia 100, ila siko tayari kubadili dini kwa ajili yake maana kwetu ni wakristo na hapa naongea mama yangu ni mzee wa kanisa hivyo Shilole naamini anaweza kubadili maana mimi tayari nimeshafanya mengi sana juu yake.” alisema Nuhu.

"Mimi siwezi kubadili dini maana Nuh ndiye alisema atabadili hata hivyo familia yangu haiwezi kunikubalia kubadili dini kwa ajili ya kufunga ndoa kama amesema naye hawezi kubadili basi tutaishi tu maana hata ndoa ya serikali yenyewe hawezi na maisha siyo lazima tuoane.”alisema Shilole.

Kutokana na majibu hayo pande zote mbili ni dhahiri kuwa wawili hao kufunga ndoa kwao ni jambo ambalo halipo.

SOURCE:GLOBAL

0 Response to "NDOA YA SHILOLE NA NUHU NI NDOTO NZITO"

Post a Comment