Latest Updates

JCB Kuachia Ngoma ya Mapenzi Mwezi HuuRappa kutoka Tazania ambae kwa sasa anaishi nchini Denmark amesema anatarajia kuachia ngoma mpya ambayo tofauti na alivozoeleka itakua ikizungumizia Mapenzi.
Rappa huyo amesema kua wakati anajianda kuondoka Tanzania kueleka huko Denmark alifanya kazi nyingi ili atakapokua nje ya nchi awe ana kazi za kutosha kwa ajili ya mashabiki wake.
Jcb amesema kua ni mda mrefu hajaandika wimbo wa mapenzi ambapo amesema kupitia wimbo huo mpya utakaoitwa' Mtoto Mkali ' utakua ukielezea jinsi alivotoka mbali na mpenzi wake kutoka maisha ya ghetto (ghetto love )mpaka  kufikia hatua ya kuwa na familia ambapo kwa wapenzi wake amesema ni wakati sahihi kuiachia mtaani.
Jcb amesema wimbo huo utatoka tarehe 10 ya mwezi huu november na imetyarishwa na mtayarishaji Daz knaledge toka Arusha

0 Response to "JCB Kuachia Ngoma ya Mapenzi Mwezi Huu"

Post a Comment