Latest Updates

BEN POL AWEKA WAZI MAHUSIANO YAKE
MSANII wa muziki miondoko ya R&B, Ben Pol ameweka wazi kuwa mahusiano pekee yaliyodumu kwa muda wa miezi 9, ni mahusiano yake ya kimapenzi na aliyewahi kuwa mshindi wa pili wa Miss Tanzania 2013, Latifa Mohamed.

Ambapo ameweka wazi kuwa hayo ndiyo mahusiano pekee aliyoweza kudumu kwa miezi 9 huku yakiendelea kuwepo huku kila mmoja akiwa na ndoto tofauti tofauti kwenye kuboresha mahusiano hayo.

Kwa mujibu wa Bongo5, Ben Pol alielezea kuwa ameshapita kwenye mahusiano tofauti tofauti na watu mbalimbali, huku akishindwa kudumu kwenye mahusiano hayo kutokana na kila mmoja kuingia na matamanio tofauti.

Alisema kuwa kuna wanaliongia katika mahusiano wakiwaza vitu vikubwa kutoka kwake hivyo alivyoshindwa kutimiza mambo hayo mahusiano yalishindwa kuendelea, lakini haya ya sasa anaona kila jambo linaenda sawa.

“Unajua unapokutana na mtu na kuingia kwenye mahusianao mwingine anawaza Ben Pol atakuwa ni mtu wa kujirusha, kwenda sehemu za starehe, kumbe ndivyo sivyo mimi ni mtu wa kukaa na kufanya mambo ya kimaendeleo zaidi hivyo bata si kw asana” alisema Ben Pol.

0 Response to " BEN POL AWEKA WAZI MAHUSIANO YAKE"

Post a Comment