Latest Updates

BELLE 9 KUTOFANYA KAZI NA DIAMOND????BAADA ya kuonekana anafanya vizuri katika soko la muziki wa kizazi kipya nchini Diamond Platinum, huku baadhi ya wasanii wakitamani kufanya naye kazi ya muziki wapo baadhi ya wasanii ambao hawatamani kufanya naye muziki kwa kile kinachoonekena kuwa hakuna muendano sawa wa kazi.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Morogoro, Belle 9 hafikirii kufanya collabo na Diamond Platinumz hivi karibuni kwa kuwa bado haoni chemistry (muendano sawa) kati yao.

Akiongea jijini Dar es Salaam, Belle 9 amesema haoni kama kuna chemistry kati yake na mwimbaji huyo ingawa haweki mipaka ya collabo kati yao, ikitokea wamepata kitu wanaweza kufanya.

“Kama ikitokea nina wimbo ambao yeye anaweza kuplay part yake vizuri tunaweza tukafanya. Ikitokea mimi nimeandika wimbo ambao nahisi kabisa yeye akikaa atafit tunaweza tukafanya. Lakini sio chemistry hapo kwanza.” Alisema Belle 9 .

Mwimbaji huyo amesema hivi sasa anafikiria kufanya kazi na mzee Zahir Zorro au Banza Stone kwa ajili ya kupata kitu cha kipekee.

“Hawa vijana wanaimba vizuri. Kiwango kipo, sijasema sioni… lakini the same. Mimi ninahitaji kitu unique kwa sababu nahisi kwa kumshirikisha Zahir au Banza Stone hivi…yaani watu ambao mimi naweza kuchukua kitu pale. Kuna watu wengi ambao naweza kujifunza vitu vingi.” Belle 9 amefafanua.

Hata hivyo, amesema wasanii wapya wa kizazi kipya wanafanya vizuri sana pia na akawataja wengi aliowashirikisha kwenye nyimbo zao kuonesha jinsi anavyowakubali.

0 Response to " BELLE 9 KUTOFANYA KAZI NA DIAMOND????"

Post a Comment