Latest Updates

Ulidata na Ole Themba? Linah anakuja na wimbo mkubwa zaidi, amshirikisha msanii mkubwa Afrika


Kama wewe ni mmoja kati ya ‘waliodata’ na ngoma ya Linah aliyofanya Afrika Kusini akiwashirikisha Uhuru, tegemea kudata zaidi na ujio mpya wa msanii huyo.
Linah ambaye hivi sasa anafanya kazi chini ya kampuni ya kimataifa ya ‘No Fake Zone’, ameiambia tovuti ya Times Fm kuwa wimbo unaofuata utakuwa mkubwa zaidi ya Ole Themba na kwamba amefanya na msanii mkubwa sana Afrika.
“Yaani inakuja kubwa zaidi ambayo hiyo itakuwa funika, waswahili wanasema itakuwa ‘ndio basi tena..’ (anacheka). Nimeshaifanya ila kuna baadhi ya vitu ambavyo naenda kumalizia. Kwa hiyo Mungu akijalia hizo wiki zinazokuja ntaenda (Afrika Kusini) kumalizia.” Linah ameiambia tovuti ya Times Fm.
Hata hivyo hakumtaja msanii huyo aliyefanya nae kazi na kuahidi kuwa itakuwa surprise baada ya kazi kumalizika na kutoka kama ilivyokuwa ‘Ole Themba’.
Katika hatua nyingine, Linah ameeleza kuwa wimbo wake Ole Themba umempa mafanikio makubwa ambayo hakuwahi kuyafikia na kwamba sio Tanzania tu bali Afrika kwa ujumla kwa kuwa video yake imechezwa katika vituo vingi sana vikubwa.
Usikose kusikiliza Bongo Dot Home ya 100.5 Times Fm Jumamosi hii kuanzia saa 10 kamili jioni utamsikia Linah akieleza mengi ikiwa ni pamoja na ufafanuzi baada ya kuchaguliwa kuwa balozi wa wanawake na Uchumi.

0 Response to "Ulidata na Ole Themba? Linah anakuja na wimbo mkubwa zaidi, amshirikisha msanii mkubwa Afrika"

Post a Comment