Latest Updates

Man Walter aeleza walipofikia katika kufanya kazi na 20 Percent


Mtayarishaji wa muziki kutoka Combination Sound, Man Walter aliwahi kutangaza kumaliza tofauti kati yake na 20 Percent aliyewahi kufanya vizuri kupitia mikono yake na kwa pamoja wakaeleza mpango wa kufanya mradi mpya.
Man Water ameongea na tovuti ya Times Fm na kueleza walipofikia baada ya ukimya wa muda mrefu tangu walipotangaza hatua hiyo.
“Off Course kwa sasa siwezi kuongelea sana kwa sababu wazo lilienda vizuri lakini nadhani kuna vitu viwili vitatu vilikwama, sijapata tena mawasiliano mazuri na 20. Labda tuvute subira tu, kwa sababu kama watu wana lengo la kufanya jema litakuwa tu…nadhani tuvute subira kwake.” Man Walter ameiambia tovuti ya Times Fm.

Amefafanua kuwa milango iko wazi kwa 20 Percent kufanya kazi kwake kwa kuwa yeye ni mfanyabiashara lakini pia anasubiri sana kufanya kazi na msanii huyo ili kuwahakikishia watu kuwa hakuna tatizo lolote kati yao.
20 Percent aliwahi kuchukua tuzo 5 katika kinyang’anyiro cha KTMA kwa kazi alizofanya na Man Walter.
Man Walter ameachia wimbo mpya hivi karibuni aliofanya mwenyewe kwa kushirikiana na Mbatizaji. Unaitwa ‘Wife Material’.

0 Response to "Man Walter aeleza walipofikia katika kufanya kazi na 20 Percent"

Post a Comment