Latest Updates

Keyshia Cole akamatwa baada kumshambulia mwanamke akimpigania Birdman


Mwimbaji Keyshia Cole amesomeka sana kwenye vichwa vya habari baada ya kuripotiwa kumshambulia vibaya mwanamke mmoja aliyedaiwa kujivinjari na Birdman.
Kwa mujibu wa TMZ, Keyshia aliingia alipokuwa boss huyo wa Cash Money huko Magharibi mwa Los Angeles, Ijumaa, majira ya saa kumi na moja alfajiri ndipo alipomkuta mwanamke huyo aliyedaiwa kuspend usiku na Birdman. Alianza kumshambulia vibaya na kumchanachana kwa makucha usoni.
Polisi walifika katika eneo hilo na kumkamata kwa kosa la jinai huku wakimtuhumu pia kwa kosa la kuendesha gari kwa uzembe kinyume cha sheria za barabarani.
Baada ya kukaa rumande saa kadhaa, aliachiwa kwa dhamana ya $ 46,000.
Muda mfupi baada ya kuwa huru Keyshia alihamia kwenye Instagram na kuandika jumbe za ajabu.
Moja kati ya jumbe hizo ilisomeka, “Ni**az be like, ‘WTF I gotta lie for’ and still be lying.”
Katika hatua nyingine, Keyshia anatarajia kuachia albam yake ya Sita ‘Point of No Return’ inatarajia kuingia sokoni October 7.

0 Response to "Keyshia Cole akamatwa baada kumshambulia mwanamke akimpigania Birdman"

Post a Comment