Latest Updates

JUSTIN BIEBER AACHA ULEVI

Mwimbaji Justin Bieber ameamua kuyaanza maisha mapya kwa kuacha kutumia vilevi na vyakula visivyoshauriwa kiafya ili kuinusuru zaidi kazi yake ya sanaa. 

Kwa mujibu wa chanzo cha gazeti la The Sun, Justin Bieber amekuwa akijigamba mbele ya marafiki zake kuhusu maisha mapya ya afya bora. 

“Hanywi tena pombe na ameacha kula vyakula visivyoshauriwa kiafya pia. Alikuwa katika wakati mgumu miezi michache iliyopita na anatumaini hii itampa mwanzo mzuri.” Kimeeleza chanzo hicho. 

Mwimbaji huyo ambaye amekuwa katika matatizo ya kisheria hivi karibuni, anaonekana kuyaanza maisha mapya katika uhusiano wake pia baada ya kutangaza kuwa yuko tayari kuwa baba na anataka kumuoa mpenzi wake Selena Gomez. 

Kupitia Instagram, Bieber amepost picha inayooashiria hatua yake hiyo na kuandika, “To start something new you have to stop something old.What are you living for? What is your calling? Set standards and boundaries #begreat.”

0 Response to "JUSTIN BIEBER AACHA ULEVI"

Post a Comment