Latest Updates

DR.DRE AONGOZA ORODHA YA FORBES YA WASANII WA HIP HOP


Daktari wa midundo, Dr Dre ameongoza orodha ya Forbes ‘Hip Hop Cash Kings 2014’ akivaa taji hilo baada ya kuingiza kiasi cha $620 million mwaka huu. 

Sio tu kwamba Dr Dre ameongoza orodha hiyo bali ameweka rekodi ya aina yake kwa kuwa kiwango alichoingiza kinazidi jumla ya fedha zote walizoingiza wasanii wengine 24 walioingia kwenye orodha hiyo mwaka huu. 

Dre anarudi kwenye nafasi yake hiyo aliyokuwa akiishikilia mwaka 2012 kabla ya kufunikwa na P. Diddy mwaka jana. 

Anaongoza orodha hiyo kwa kishindo baada ya kampuni ya Apple kutangaza kuinunua kampuni anayoimiliki kwa kushirikiana na Jimmy Lovine ya Beats Electronics kwa $3 billion. 

Nafasi ya pili imeshikiliwa na Jay Z na P.Diddy ambao wamefungana kwa kuingiza kiasi cha $60 million kila mmoja. 

Jay Z ameingiza kiasi hicho kupitia matamasha mengi aliyoyafanya, biashara zake na album yake ya Magna Carter Holy Grail iliyofikia mauzo ya Platinum hata kabla haijaachiwa baada ya kampuni ya Sumsang kununua nakala milioni moja. 

P. Diddy yeye aliingiza kiasi hicho ($60 million) kupitia biashara zake mbalimbali ikiwa ni pamoja na mradi wake wa mavazi wa Sean Jean, Revolt TV na mengine.

Angalia orodha kamili: 

Dr Dre- $ 620 Million
Jay Z- $60 Million (tie)
Diddy- 60 Million (tie)
Drake – 33 Million
Macklemore & Ryan Lewis 32 Million
Kanye West- 30Million
Birdman – 24Million
Lil Wayne- 23Million
Pharell William -22Million
Eminem- 18Million
Nicki Minaj- 14Million
Wiz Khalifa- 13Million (tie)
Pitbull- 13Million (tie)
Snoop Dogg- 10Million
Kendrick Lamar- 9Million
Luda Cris – 8Million (tie)
Tech N9ne- 8Million (tie)
Swizz Beatz -8Million (tie)
50 Cent- 8Million (tie)
Rick Ross- 7Million (tie)
J. Cole –7Million (tie)
DJ Khaled- 7Million (tie)
Lil Jon- 7Million (tie)
Mac Miller -7Million

0 Response to "DR.DRE AONGOZA ORODHA YA FORBES YA WASANII WA HIP HOP"

Post a Comment