Latest Updates

AY awapa mbinu rahisi wachezaji wa Tanzania kupata nafasi klabu kubwa duniani


Msanii wa Bongo Flava, Ambwene Yesaya ametoa mbinu mpya na rahisi kwa wachezaji nchini Tanzania kutumia teknolojia ya mtandao kujitangaza kimataifa.
Akiongea katika kipindi cha Maskani cha 100.5 Times Fm wakati wakifanya mjadala wa michezo na Gardner Habash na Clifford Mario Ndimbo, AY aliwashauri wachezaji wa Tanzania kuhakikisha wanaweka vipande vya video za mechi au sehemu walizocheza vizuri zaidi ili kujipa nafasi ya kuangaliwa na dunia nzima.
Alieleza kuwa ligi za hapa nyumbani ni vigumu kuangaliwa na wadau wakubwa wa mpira duniani lakini kwa kutumia channel za Youtube ni rahisi watu hao kuangalia video zao hata baada ya muda mrefu kupita na wanaweza kuvutiwa na uchezaji wao.
Aliongeza kuwa aliwahi kuzungumza na rafiki yake mmoja kutoka Uingereza ambaye ana nafasi katika timu ya Manchester United na akajaribu kumdadisi kama wanaweza kufanya mpango wa kuona vipaji vya wachezaji kutoka Tanzania lakini swali moja tu lilikuwa jibu tosha.
“Aliniuliza ‘kuna channel za YouTube za wachezaji wa Tanzania ambazo tunaweza kuona kazi zao?.”
Naye Clifford Mario Ndimbo ambaye ni mtangazaji wa kipindi cha Wizara ya Michezo cha 100.5 Times Fm na pia mtangazaji wa Super Sport alitoa ushuhuda kuwa kuna wachezaji ambao baada ya kuulizwa kuhusu clips za video zao ndipo humtafuta kumuomba kama ana video nzima ya mechi ya kipindi fulani ili wazitumie.

0 Response to "AY awapa mbinu rahisi wachezaji wa Tanzania kupata nafasi klabu kubwa duniani"

Post a Comment