Latest Updates

Papa Francis atabiri kifo chake


Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis ametabiri hatima ya maisha yake hapa duniani ikiwa ni mwaka mmoja tangu aachiwe kiti hicho na Papa Benedict XVI aliyeng’atuka kutokana na matatizo ya kiafya.
Akiongea na waandishi wa habari kwenye ndege wakati akirejea Vatican kutoka ziarani nchini Korea Kusini, Papa Francis amesema kuwa suala la kuendelea kuishi ni neema ya Mungu na kwamba atafariki baada ya miaka miwili au mitatatu.
“Suala hili naliona kama neema tu ya Mungu kwa watu wake. Najaribu kutafakari kuhusu dhambi zangu na makosa yangu, siwezi kujivuna. Najua kwa sababu hali hii itadumu kwa muda mchache. Miaka miwili au mitatu nitakuwa nimeondoka na kwenda nyumbani kwa baba.” Amesema Papa Francis.
Ingawa Papa Francis mwenye umri wa miaka 77 hajawahi kuzungumza hadharani kuhusu suala la afya yake, lakini baadhi ya vyanzo vya habari kutoka Vatican vimeeleza kuwa amekuwa akiwaambia watu wake wa karibu kuhusu siku zake chache zilizosailia dunia.
Wachambuzi wa masuala ya kiimani wameeleza kuwa huenda Papa Francis ana tatizo la kiafya ambalo hakuliweka wazi.
Chanzo: Mwananchi

0 Response to "Papa Francis atabiri kifo chake"

Post a Comment