Latest Updates

Godzilla azungumzia video ya wimbo wake na G-Nako 'Tumewaka' na mpango wa kufanya Project ya pamoja


Rapper wa SalaSala, Gozilla amezungumzia mpango wa kuuweka kwenye runinga wimbo waliofanya na Mweusi G-Nako ‘Tumewaka/Umenisoma’.
Akiongea na The Jump Off ya 100.5 Times Fm, Godzilla amesema wana mpango wa kushuti video hiyo jijini Arusha mara baada ya G-Nako kumaliza mishe zake.
“Tumewaka tulitaka kuishuti sema G. anaratiba za show alienda Mbeya. Tulipeana muda I think wiki hii au wiki ijayo tutaishuti, tutaenda kuishutia A-Town. G. amenambia ameshaongea na director fresh (sijamjua), lakini G. namuaminia kwenye kazi.” Amesema Godzilla.
Akiongelea mpango wa kufanya mradi wa pamoja au kazi nyingine, amesema tayari wameshaongea kuhusu hilo kwa kuwa kila mmoja bado ana kiu ya kufanya kazi zaidi na mwenzake lakini bado hawajajua rasmi wataifanya lini.
“Mungu ndio ana panga, lets see what’s gonna happen. Ikitokea tena tutafanya, lakini tuko na mpango huo pia wa kufanya lakini hatuwezi kupredict kesho itakuwaje au kesho italeta nini kwa sababu hatujui kesho ina nini kwenye store. We just work. Lakini pia tulikuwa na mpango wa kufanya kazi nyingine.”
Tumewaka/Umenisoma imetayarishwa na Tidd Hotter ndani ya studio za One Love FX, jijini Mwanza.

0 Response to "Godzilla azungumzia video ya wimbo wake na G-Nako 'Tumewaka' na mpango wa kufanya Project ya pamoja"

Post a Comment