Latest Updates

wasanii wa 'Original Comedy' wageuka wahudumu wa mgahawa waliouanzisha


Maonesho ya 38 ya sabasaba yanaendelea katika eneo la Sabasaba, Dar es Salaam. Makampuni, vikundi na watu mbalimbali wamefika kwa wingi kuonesha bidhaa zao kwa mtindo utakaowawezesha kuwa karibu zaidi na wateja wao.
Kundi la Ucheshi la ‘Original Comedy’ linaloundwa na wachekeshaji kama Joti, Masanja Mkandamizaji, Wakuvanga, Mpoki na Mack Regani limeanzisha mgahawa halisi kwenye maonesho hayo ambapo wasanii wa kundi hilo ndio wahudumu.
Wakizungumza na 100.5 Times Fm, wasanii wa kundi hilo wamesema kuwa wamefanya hivyo kwa lengo la kuonesha biashara yao, kuwa karibu zaidi na mashabiki wao na kwamba wanaendelea kuwahudumia na kupiga nao picha kwa muda wote watakaokuwa katika maonesho hayo.
100.5 Times Fm iko katika eneo hilo ikirusha matangazo yake LIVE na watu wanaendelea kutuma salaam moja kwa moja kwa wapendwa wao kutoka katika viwanja vya Sababa.
Ukifika katika eneo hilo, tafuta eneo lilipo gari la 100. Times Fm utahudumiwa na kuelekezwa kinachoendelea.

0 Response to " wasanii wa 'Original Comedy' wageuka wahudumu wa mgahawa waliouanzisha"

Post a Comment