Latest Updates

CHANZO CHA KUPATANA WEMA NA KAJALA CHABAINIKA


WADADA waigizaji wa bongo movies, Wema Sepetu na Kajala inadaiwa kuwa wawili hao wamemaliza tofauti zao zilizodumu kwa muda wa miezi kadhaa. 

Ambapo wawili hao inadaiwa kuwa walikuwa kama chui na paka huku sababu ya ugomvi wao kutowekwa wazi . 

Kwa mujibu wa ripoti, wasanii hao waliurudisha urafiki wao uliokuwa umetiwa doa na ‘pesa’ baada ya kukutana kwenye sherehe ya kibao kata cha mwandishi wa magazeti ya Globalpublishers. 

Baada ya sherehe hizo. Wema alipost picha inayomuonesha akiwa na Kajala, Aunt Ezekiel na wengine na kuandika, “Mwapenda sana hawa apa,.Jana hiyo kwa kibao kata cha imeldamtema….Ramadhan Qareem everebadi…” 

Pamoja na hilo juzi kwenye akaunti ya Instagram ya @kajalacelebrity2014 ambayo bila shaka ina uhusianona muigizaji huyo, imewekwa picha ya ya zamani ya inayomuonesha Kajala akiwa na Wema Sepetu na Prezzo na kuandika ‘Tbt’. Na ikaimention akaunti halisi ya Kajala

0 Response to "CHANZO CHA KUPATANA WEMA NA KAJALA CHABAINIKA"

Post a Comment