Latest Updates

Video ya wimbo wa Shetta 'Kerewa' kuchezwa Trace na Channel O


Tegemea kuiona video ya wimbo wa Shetta aliomshirikisha Diamond ‘Kerewa’ kwenye vituo vingine vikubwa vya kimataifa baada ya kuonekana jana na leo katika kituo cha MTV Base.
Shetta ameiambia tovuti ya Times Fm na kipindi cha The Jump Off kuwa tayari kampuni ya Godfather Production iliyotengeneza video hiyo imemwambia kuwa imekubalika na itaanza kuoneshwa kwenye kwenye kituo cha Trace na Channel O.
“Kesho wanaweza kuitumia Trace…hii ni station ambayo iko Ufaransa, wanaweza kuanza kuipiga according to Godfather ambaye ameniambi na  Channel O pia. Sound City ya Nigeria wameshaanza kupiga. “ Amesema Shetta.
Ameongeza kuwa station nyingi za kimataifa zimeshapewa video hiyo kwa hiyo watu wategemee kuiona pengine pia.
Rapper huyoa ameeleza kuwa hii inatokana na matunda ya kuwekeza zaidi ya Million 25 kufanya video hiyo bila kuogopa.
Usikose kusikiliza The Jump Off ya 100.5 Times Fm leo kuanzia saa mbili kamili usiku kusikiliza mengi pamoja na kumsikiliza Shetta akifafanua kuhusu taarifa hizi.

0 Response to "Video ya wimbo wa Shetta 'Kerewa' kuchezwa Trace na Channel O"

Post a Comment