Latest Updates

Tembo Nelly aipeleka Ujerumani hatua ya nusu fainali dhidi Ufaransa


Wakati mashabiki wa soka duniani wakiusubiri kwa hamu kubwa mchezo wa hatua ya robo fainali kati ya Ujerumani dhidi ya Ufaransa, vimbwanga vya kuelekea katika mchezo huo vinaendelea kushika kasi.
Mashabiki wa soka wa kila upande wanaamini ndio wenye nafasi kubwa ya kuibuka kidedea katika mchezo huo ,ambao unazikutanisha timu ambazo ni miongoni mwa timu zinazopewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa mwaka huu.
Mashabiki wa soka wa timu ya Ufaransa kwa nyakati tofauti wamezungumza na vyombo vya habari duniani kote na kueleza hisia zao za kutaka kuona upande wanaoushangilia, unaibuika kidedea na kutinga kwenye hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.
Kwa upande wa mashabiki wa soka wa Ujerumani wao wamefika mbali zaidi kwa kuonyesha hisia zao kwa vitendo, ambapo wanaamini hatua hiyo itawaminisha mashabiki wengi duniani, ni wazi upande wao utaibuka kidedea.
Mashabiki wa Ujerumani wamediriki kumtumia tembo kwa kutabiri mchezo huo ambao utachezwa kwenye dimba la Estádio do Maracanã, mjini Rio de Janeiro.
Tembo huyo aliyepewa jina la Nelly, ametabiri mchezo huo kwa kuonyesha kikosi cha Ufaransa kitapoteza mchezo wake wa hatua ya robo fainali dhidi ya Ujerumani kwa kupiga mpira ulioingia kwenye goli lenye bendera ya nchi hiyo.

0 Response to "Tembo Nelly aipeleka Ujerumani hatua ya nusu fainali dhidi Ufaransa"

Post a Comment