Latest Updates

BEYONCE ATUMIA LUGHA YA PICHA


Beyonce Knowles ameamua kutoa majibu ya taarifa zinazotajwa na vyanzo mbalimbali vya karibu kuwa yeye na Jay Z wako katika wakati mgumu wa ndoa wanaweza kuachana muda wowote.

Mwimbaji huyo wa Drunk In Love ametumia lugha ya picha kuonesha kuwa yaliyosemwa ni tofauti na maisha wanayoishi. Kupitia Instagram, July 21 Queen Bey amepost picha inayoonesha yeye na Jay Z wakiwa wameshikilia mikono ya blue Ivy anaebembea kati yao kama ishara ya kuwepo furaha katika familia hiyo.

Ingawa hakuandika chochote, picha pekee inajieleza kuwa ‘hakuna matata’ na wako kwenye wakati mzuri.

0 Response to " BEYONCE ATUMIA LUGHA YA PICHA"

Post a Comment