Latest Updates

Profesa Jay azungumzia video ya 'Tatu Chafu' aliyojishirikisha mwenyewe, 'So international'


Profesa Jay amepanga kuwapa mashabiki wake zawadi ya siku kuu ya Eid wakati ambapo wanajiandaa kupata video ya wimbo wa Kipi Sijasikia.
Akiongea   rapper huyo mkongwe amesema hivi karibuni anatarajia kuachia wimbo mwingine mpya alioupa jina la ‘Tatu Chafu’ aliojishirikisha mwenyewe kwa majina matatu tofauti yenye style tatu tofauti za kurap.
Humo ndani itakuwa Profesa Jay, Feat. J Hustle na Nigga J.
 “Zamani nilikuwa naitwa J Hustle, wakati nafanya muziki wangu katika hali ya u-underground kabisa maskani Kimara huko ambako tulikuwa tukitembea kwa miguu muda mwingi sana kutafuta Party na Shows….lakini baadae nilibadili jina na kuitwa Nigga J. Wengi hawamjui J Hustle, wengi wanamjua kuanzia Nigga J. Kwa sababu Nigga J ni yule aliyeingia Hard Blasters tukachukua ubingwa wa Hip Hop Bongo mwaka 1995, tukatoa Chemsha Bongo na vitu kama hivyo.
“So Tatu Chafu imeunganisha vichwa vitatu. Ni kichwa kimoja lakini kimegawanyika kwenye bongo tatu tofauti. Kwa hiyo kuna J Husle, Nigga J na Profesa Jay ambaye anaongea hapa.” Amesema Profesa Jay.
Profesa hataki kukaa kimya tena na sasa anaachia kitu baada ya kitu na ameamua kufanya video ya wimbo wa Tatu Chafu na muongozaji Hefemi ambaye ni Mtanzania anaefanyia kazi zake nyingi Marekani.
Hefemi aliyefanya video ya Historia ya Lady Jay Dee na Sumu Ya Panya/My City ya rapper Wakazi.
“Nategemea kuanza kushuti video ya Tatu Chafu Jumatatu ambayo tutaishuti na bonge la producer kutoka US anaitwa HEFEMI, kila kitu kiko kwenye pipeline. So tulikuwa tunaangalia tuache watu wale sikukuu kidogo tuanze kushuti Tatu Chafu na Hefemi. So international kama nilivyoahidi, watu wategemee vitu vikubwa.”

0 Response to "Profesa Jay azungumzia video ya 'Tatu Chafu' aliyojishirikisha mwenyewe, 'So international'"

Post a Comment