Latest Updates

Ajidai mgeni wa Eid na kumuua ndugu wa rais wa Afghanistan


Mtu aliyekuwa amevaa bomu kwa siri amemuua ndugu wa rais wa Afghanistan,  Hamid Karzai kusini mwa jiji la Kandahar.
Maafisa wameelezaa kuwa Hashmat Karzai alikuwa anapokea wageni katika nyumba yake walioleta salam za Eid, ndipo mtu huyo alipojilipua na kumuua yeye pia.

Ndugu huyo wa rais Hamid anaefahamika kwa jina la Hashmat Karzai alikuwa meneja kampeni wa Ashraf Ghani ambaye ni mmoja kati wagombea wawili wa urais wanaopewa nafasi kubwa ya kukikalia kiti cha Hamid Karzai baada ya uchaguzi.
Hakuna kundi lolote lilidai kuhusika na mauaji hayo. Kundi la Taliba limekuwa likijihusisha na mauaji katika jiji hilo wakati ambapo wakielekea kwenye uchaguzi wa rais

0 Response to "Ajidai mgeni wa Eid na kumuua ndugu wa rais wa Afghanistan"

Post a Comment