Latest Updates

MUME WA FLORA MBASHA APATA DHAMANA


MFANYABIASHARA maarufu ambaye pia ni muimbaji wa nyimbo za Injiri ambaye ni Mume wa Flora, Emmanuel Mbasha anayekabiliwa na kesi ya ubakaji yupo nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana ambayo yaliyowekwa na mahakama ya Wilaya ya Ilala. 

Mume wa Flora, Emmanuel Mbasha ambaye anakabiriwa na kesi hiyo ya ubakaji amepata dhamana leo baada ya kutimiza masharti ya dhamana yaliyowekwa na mahakama hiyo ya Wilaya ya Ilala. 

Ambapo moja ya sharti hilo la Dhamana ni kuwa na wadhamini wawili ambao wote wawe wanafanya kazi katika taasisi inayotambulika kisheria . 

Ambapo June 17 mwaka huu Mbele ya hakimu Willbaforce Rwago wa mahakama hiyo mwendesha mashtaka wa serikali Nassoro Katuga ilidaiwa kuwa mshatakiwa alitenda kosa hilo Mei 23 mwaka huu eneo la Tabata Kimanga. 

Bwana Emmanuel Mbasha alifikishwa mahakamani hapo na kukana shitaka la kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 17 anaedaiwa kuwa shemeji yake, na alipelekwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana. 

Muendesha mashitaka wa serikali alieleza Mahakamani hapo kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika., na kupangwa kutajwa tena July 17 mwaka huu. 

0 Response to "MUME WA FLORA MBASHA APATA DHAMANA"

Post a Comment