Latest Updates

KUNDI LA DESTINY'S CHILD WAIMBA NYIMBO YENYE MAADHI YA KIAFRIKA


Afrika inaendelea kuwa mfano mzuri wa kuigwa na wasanii wakubwa duniani, hii ina maanisha wasanii wa Afrika waendelee kufanya nyimbo za kiafrika zaidi ili kuendelea kupenya na kukubalika huko Ughaibuni. 

Kama unakumbuka Beyonce aliwahi kusema kuwa mtindo wa kucheza na mdundo wa hit yake ‘Who Run The World/Girls’ aliuchukua Afrika na hata akaamua kuwatafuta hao waafrika na kuwashirikisha kwenye video ya wimbo huo. 

Sasa member mwingine wa Destiny’s Child, Michelle amewaliunganisha kundi hilo kwa wimbo wenye ujumbe wa injili aliupa jina la ‘Jesus Say Yes’. 

Michelle aliuachia rasmi jana wakati anafanya interview na kipindi cha Good Morning Amerika na akaeleza kuwa aliusikia wimbo wa Nigeria wenye mahadhi hayo akaupenda na akaamua kuufanya yeye kwa heshima. 

“Ilikuwa furaha sana. Ilikuwa kama watoto wadogo tena. Ninawalinda wananilinda pia. Wameonesha imani kubwa kwangu muda baada ya muda.” Alisema Michelle. 

Video inawaonesha waimbaji hao wakiwa katika mavazi ya heshima na wachezaji wao wanaakisi mitindo na mavazi ya Afrika.

0 Response to "KUNDI LA DESTINY'S CHILD WAIMBA NYIMBO YENYE MAADHI YA KIAFRIKA"

Post a Comment