Latest Updates

MAFIKIZOLO WAMZUNGUMZIA DIAMOND PLATINUMZ..


                           
Wanasema safari moja huanzisha nyingine... na kweli ile safari ya Diamond iliyoanzia kwa Davido kuanza kukolabo na mastaa wa kimataifa imezaa nyingine.Pamoja na kwamba mpaka sasa Diamond ameshafanya kolabo na mastaa wa Nigeria kama Iyanya, Davido na Tiwa Savage, Mtanzania huyu amepata nafasi ya kuingia kwenye soko la Afrika Kusini baada ya kualikwa na kundi la Mafikozolo.

Kwenye utoaji wa tuzo za MTV Africa Music Awards au MAMAs zilizofanyika 7 June jijini Durban, South Africa, Mafikizolo waliomba kumshirikisha Diamond kwenye wimbo wao mpya ambao wamefanikiwa kuurekodi June 9 usiku kwenye studio za mkongwe Oskido kule JohannesburgBaada ya kurekodi hiyo kolabo, Theo wa Mafikizolo alisema: "Diamond ni mwepesi tofauti na nilivyotarajia, huyu ni miongoni mwa wasanii wa Africa tunaowataka, lengo letu ni kuufikisha muziki kwenye kila kona ya Afrika na ndio maana tumeomba kufanya kolabo na huyu staa wa Afrika Mashariki." 


Kwenye sentensi ya mwisho ya exclusive interview na DStv.com, Theo amesema walimfahamu Diamond Platnumz kupitia kwa Davido, yaani walimuuliza Davido ni nani mkali wa Afrika Mashariki kwa sasa akawaambia Diamond.

0 Response to "MAFIKIZOLO WAMZUNGUMZIA DIAMOND PLATINUMZ.."

Post a Comment