Latest Updates

DAYNA NYANGE NA NANDO JE NI WAPENZI ?


MWIMBAJI wa Nivute kwako Dayna Nyange amezungumzia uhusiano wake na mshiriki wa Big Brother Africa, Ammy Nando baada ya kuonekana katika picha kadhaa wakiwa katika poz tata.Dayna amefunguka hayo kupitia mahojiano aliyafanya jijini Dar es Salaam na kuelezea ukaribu wao na kinachoendelea.

“Jamani Nando ni rafiki yangu, hakuna kitu serious,  he’s just a friend tu basi.Sijui nisemeje, ni watu ambao tumefahamiana si kwa muda mrefu sana lakini tumeshibana so imekuwa hivyo tumekuwa karibu mara kadhaa. Haipiti muda mrefu bila kuonana kwa hiyo mara nyingi tunakuwa wote. Ninamkampani kwenye issue zake na yeye ananikampani pia mimi, ni watu ambao tumekuwa karibu sana kwa kweli.” alisema Dayna.

Alipoulizwa kuhusu picha zao zinazoonekana kwenye Instagram ambazo zinaongea zaidi ya urafiki, alifunguka na kudai kuwa kwa kuwa wao ni marafiki wa karibu imekuwa  raisi kupiga picha hizo kwa ukaribu.

“Yeah...sasa mtu na rafiki yake si mnapiga picha mnakuwa free jamani…hivyo (kicheko).”

Hata hivyo, Dayna amesema kuna kitu ambacho wanakifanya pamoja na kitakapokuwa tayari watu watafahamu.

0 Response to "DAYNA NYANGE NA NANDO JE NI WAPENZI ?"

Post a Comment