Latest Updates

Marekani yatangaza vikwazo dhidi ya Uganda kwa kupinga ushoga

Afisa uhusiano wa Marekani anaeshughulikia masuala ya usalama katika ikulu  ya Marekani, Caitlin Hayden ameweka wazi vikwazo hivyo kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari.
Amesema sheria hiyo inakiuka haki za binadamu, hivyo Marekani imeamua kuwapiga marufuku wanahakati walioshiriki katika kuipitisha sheria hiyo kutoingia tena Marekani.
Ameongeza kuwa Marekani itasitisha ushirikiano wake na jeshi la polisi la Uganda na Wizara ya Afya, na pia itasitisha mazoezi ya pamoja kati ya wanajeshi wa Marekani na wale wa Uganda.
Hii inamaanisha kuwa Marekani itajitoa katika juhudi za kumtafuta Joseph Koni kama walivyokuwa wamekubaliana na serikali ya Uganda.
Sheria dhidi ya mapenzi ya jinsia moja iliyopitishwa na bunge la Uganda inatoa adhabu ya kifungo cha maisha kwa mtu atakayekutwa na hatia ya kujihusha na mapenzi ya jinsia moja.

0 Response to "Marekani yatangaza vikwazo dhidi ya Uganda kwa kupinga ushoga"

Post a Comment