Latest Updates

JOH MAKINI KUACHIA ' I SEE ME'



MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini miondoko ya Hip Hop, Joh Makini 'Mweusi'anatarajia kuachia wimbo mpya hivi karibuni.Ambapo ametangaza kuachia wimbo wake mpya Jumanne, June 24 wimbo alioupa jina la ‘I See Me’ na umetayarishwa na Nahreel.

I See Me ni wimbo ambao aliwahi kuwasikiliza watu waliohudhuria kwenye uzinduzi wa video ya wimbo wa Gere ya Weusi ambapo anasikika akijieleza kuwa anajiona mbali hata akimvuka Wale wa Marekani.

Akizungumza katika mahojiano na jarida hili, Joh Makini alibainisha kuwa wimbo huo anatarajia kuachia siku hiyo ambayo anaamini utapokelewa vyema na mashabiki wake.

"Sijui kama nilishawahi kuaribu kwenye nyimbo yangu yoyote, hivyo naamini hata hii ninayoitoa itafanya vizuri kwenye ulimwengu wa soko la muziki ndani na nje ya nchi" alisema Joh Makini.

0 Response to "JOH MAKINI KUACHIA ' I SEE ME'"

Post a Comment