Latest Updates

Filamu ya maisha ya Aaliyah yapata pigo, Mrembo aliyechaguliwa kuigiza kama Aaliyah ajitoa


Filamu ya maisha ya Aaliyah iliyokuwa inaandaliwa na kampuni ya Lifetime imepata pigo baada ya muigizaji wa kike Zendaya Coleman aliyekuwa amepangwa kuigiza kama Aaliyah kujitoa katika filamu hiyo.
Muwakilishi wa Zendaya Coleman ameeleza kuwa muigizaji huyo ameamua kujitoa baada ya kugundua kuwa Lifetime bado hawajapata haki kisheria ya kufanya filamu au hata kutumia kazi yoyote ya muziki ya Aaliyah.
Baada ya kutangazwa kuwa Lifetime wamepanga kufanya filamu ya maisha ya Aaliyah. Kundi la watu waliojitambulisha kuwa mashabiki wa kweli wa marehemu Aaliyah waliandika Petition kupinga hatua hiyo kwa kuwa hakukuwa na idhini ya familia ya marehemu kuhusu mpango huo.
Mjomba wake Aaliyah pamoja na Meneja wake Barry Hankerson walipaza sauti wakiwataka Lifetime kusitisha mpango wao kwa madai kuwa filamu hiyo itakuwa na heshima ndogo sana kwa Aaliyah.
Zendaya aliweka wazi pia mpango wake wa kutoshiriki filamu hiyo endapo hakutakuwa na haki.

0 Response to "Filamu ya maisha ya Aaliyah yapata pigo, Mrembo aliyechaguliwa kuigiza kama Aaliyah ajitoa"

Post a Comment