Latest Updates

Diamond azungumzia tuhuma za kuiba nyimbo ikiwemo Kitorondo (MdogoMdogo)


Pichani: Jabir Saleh na Diamond
Karibu kila mwaka kumekuwa na malalamiko ya wasanii kuhusu kuibiwa nyimbo au idea za nyimbo zao na Mkali wa Ngololo Style, Diamond Platinumz, madai ambayo huzua hisia tofauti kwa watu wengi.
Hivi karibuni, mshiriki wa BSS Wababa naye alijitokeza na kudai kuwa Diamond amemuibia wimbo wake wa Kitorondo na kwamba baadae aliubadilisha jina na kuuita MdogoMdogo.
Diamond amezitolea majibu tuhuma hizo jana (June 25) wakati akifanya mahojiano na Jabir Saleh katika kipindi cha The Jump Offf cha 100.5 Times Fm.
“Unapokuwa mkubwa sana kunakuwa kuna faida yake na madhara yake. Na madhara yake yalivyo, unapokuwa mkubwa sana kitu ambacho hakina maana watu wanajaribu kukifanya kuwa na maana, either kionekane kizuri au kibaya.”Amesema Diamond.
 Mfano nilipotoa Moyo wangu nyimbo nyingi sana zilitoka zinaitwa Moyo Wangu. Lakini hujawahi kusikia hata siku moja nikasema kuna mtu kaniibia. Kwa sababu lile ni neno ambalo wewe unavyojua wewe na mimi nikatumia ninavyojua mimi kwa sababu hakuna mwenye maneno yake duniani.” Alifafanua.
Akizungumzia tuhuma zilizotolewa na msanii Wababa hivi karibuni kuwa alimuibia wimbo wake wa Kitorondo na baadae akaubadili kuwa Mdogo Mdogo, Diamond amesema huo ni wimbo wa Asili ambao ulikuwa unaimbwa na bendi ya Tandale Modern Taarabu, na pia ni ngoma ya mdundiko wa zamani.
“Sitaki niongee kwa sababu nitampa Kick…anyways nilisikia kuna mtu anasema eti hii nyimbo yangu ya MdogoMdogo kuna mtu kaibiwa kwa neno la Kitorondo. Sasa mimi nikuadithie story fupi...mimi nimezaliwa Tandale nimekulia Tandale, kuna bendi ilikuwa inaitwa Tandale Modern Taarab nyimbo yao ya kwanza inaitwa Tandale (anaimba kidogo). Ukiacha hivyo, Kitorondo ni jina ambalo ni ngoma ambayo wanaimba hivyo (anaimba). Yaani hii ni nyimbo.
“Kuna msanii kaichukua kaiimba kama ilivyo ile nyimbo ya mdundiko. Halafu baada ya kusikia neno la Kitorondo kwenye nyimbo yangu akasema yeye kaibiwa nyimbo. Mimi nimepata taarifa nikasema ana akili kweli. Yeye ndio kaenda kuiba. Mimi nimetumia neno la Kitorondo kwa taaluma zangu za kimuziki naliingiza kwa namna gani kama neno, yeye anasema nimemuibia yeye. Sikujisikia vizuri…halafu nikaulizwa kila sehemu nikienda nawaambia msiniulize maswali hayo kabisa.”
Diamond alizungumzia masuala mengi ikiwa ni pamoja na maandalizi ya Tuzo za BET ambapo anategemea kuwa na mkutano wa kimataifa kwa ajili ya tuzo hizo huko Marekani, mkutano utakaowajumuisha wasanii wengi wa kimataifa kama project ya dunia nzima

0 Response to "Diamond azungumzia tuhuma za kuiba nyimbo ikiwemo Kitorondo (MdogoMdogo)"

Post a Comment